Amebaini kuwa na hadathi baada ya swalah

Swali: Afanye nini mtu ambaye ameswali kisha baada ya swalah ikabainika kwamba yuko na hadathi inayowajibisha kuoga?

Jibu: Kila mtu anayeswali kisha baada ya kumaliza kuswali ikambainikia kuwa yuko na hadathi kubwa au hadathi ndogo, italazimika kwake kujitwahirisha kutokamana na hadathi hii na arudi kuiswali swalah yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah haikubali swalah bila twahara.”[1]

[1] Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 299
  • Imechapishwa: 05/05/2020