Ameapa kuwa havuti tena sigara ila akavuta


Swali: Mtu akiapa kuwa hatovuta sigara kisha akavuta. Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Ni lazima kwake kutubu na kutoa kafara ya kiapo ambapo atatakiwa kuwalisha masikini kumi, asipoweza aache mtumwa huru, asipoweza afunge siku tatu pamoja vilevile na kutubu na kuomba msamaha. Msingi ni kwamba anatakiwa kuacha sigara hata kama hakuapa. Kwa sababu ni katika vichafu na ni yenye kudhuru afya na kuharibu mali na mwili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 11/08/2018