Ameanza kufunga Shawwaal kabla ya Ramadhaan kwa kusahau


Swali: Nilifunga Ramadhaan na himdi zote ni Zake Allaah. Lakini nikala siku moja kwa sababu ya safari. Baada ya Ramadhaan nikaanza kufunga siku sita za Shawwaal. Baada ya kupita siku tatu ndipo nikakumbuka kuwa nadaiwa siku moja. Ni ipi hukumu? Nifanye nini?

Jibu: Kwa hali yoyote mtu akianza kufunga masiku sita ya Shawwaal huku amesahau kuwa anadaiwa, pale atapokumbuka afunge yale masiku anayodaiwa kisha akamilishe zile siku sita. Kwa sababu mpangilio hapa umeanguka kwa kusahau. Mpangilio unaanguka kwa kusahau.

Lakini ikiwa amenuia siku hii kuwa ni ya Shawwaal hawezi kuifanya ikawa ni deni lake alilolipa. Kwa sababu siku anayotakiwa kulipa ni lazima ainuie kabla ya Fajr.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: l-Liqaa´ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/939
  • Imechapishwa: 08/05/2018