Swali: Kuna baadhi ya watu wamenialika nije kutoa kalima katika mnasaba wa sherehe ya mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo nikaitikia na nikatoa kalima. Je, nina dhambi kwa kufanya hivo au nazingatiwa ni miongoni mwa waliosherehekea pamoja nao?

Jibu: Ukienda kwao, ukawanasihi, ukawatolea kalima ambayo ukawaonya kutokamana na jambo hilo na ukaenda na usishirikiane nao katika yale wanayofanya kwa njia ya kwamba wasiendelee juu ya Bid´ah yao na juu ya kitendo chao, kitendo cha wewe kwenda na kuwanasihi na ukawabainishia kwamba jambo hilo halijuzu, umefanya vizuri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 10/11/2019