Swali: Miaka mingi ya nyuma nilihiji nikiwa na watoto wachanga wawili. Kwa sababu ya msongamano mkubwa kwenye Twawaaf-ul-Ifaadhwah nikachelea juu ya wana wangu wawili hawa ambapo sikukamilisha Twawaaf yangu na hivyo hajj yao haikutimia, pamoja na kwamba nilhirimia nao hajj. Je, kuna kinachonilazimu?

Jibu: Ni lazima ukamilisha hajj. Rudi ukakamilisha hajj. Ikiwa walikosa Twawaaf-ul-Ifaadhwah na Sa´y, rudi na ufanye mambo hayo mawili. Hapo hajj yao itakuwa imetimia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (20) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-6-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 25/01/2020