Ambao hawakufikiwa na Da´wah mpaka hii leo


Swali: Ni ipi hukumu ya wale ambao hawakufikiwa na Da´wah mpaka hii leo?

Jibu: Hao sio waislamu wala sio makafiri. Jambo lao liko kwa Allaah. Wao ni katika Ahl-ul-Fatrah.

Swali: Lakini ikiwa anaishi kati ya waislamu?

Jibu: Ambaye amefikiwa na Uislamu hatopewa mtihani. Hoja imekwishamsimamia kwa Qur-aan na Sunnah. Lakini jambo lake liko kwa Allaah.

Swali: Hivi leo wako watu ambao wanakufa na hawakufikiwa na Da´wah?

Jibu: Ndio, wako katika baadhi ya sehemu za Afrika na kwenginepo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 124
  • Imechapishwa: 25/08/2019