Allaah Yuko Juu Ya ´Arshi Na Uso Wake Uko Mbele Ya Mwenye Kuswali


Swali: Vipi kujumuisha kati ya Allaah Amelingana juu ya ´Arshi na kwamba Uso Wake uko mbele ya mwenye kuswali?

Jibu: Uko mbele yake wakati Yuko juu kwenye ´Arshi Yake. Yuko mbele ya mwenye kuswali wakati Yeye (Subhanaahu wa Ta´ala) Yuko juu ya ´Arshi. Allaah Halinganishwi na viumbe Vyake. Anauweka Uso Wake vile Atakavyo (Subhaanah). Yeye juu ya kila kitu ni muweza. Suala hili linahusiana na namna. Sisi hatujui namna.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mqirwani--14340317.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015