Allaah Mwenyewe ndiye kasema yuko juu mbinguni


Swali: Wakati tunapowaambia kwamba Allaah yuko juu wanasema kwamba tusimfanyie ukome Allaah kwa kuweko sehemu. Tuwaraddi vipi watu hawa?

Jibu: Haya ni maneno batili. Allaah (Jalla wa ´Alaa) yuko juu ya mbingu, kama alivyosema Mwenyewe:

أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

“Au mnadhani mko katika amani na Aliyeko juu ya mbingu kwamba hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu?”

Yeye Mwenyewe ndiye kasema kuwa yuko juu ya mbingu (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' al-Maftuuh fiy Masjid Qubaa' http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17626
  • Imechapishwa: 01/04/2018