Allaah kujitakasa na mapungufu yote kama kuchoka

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ

“Ametukuka Allaah, mfalme wa haki. Hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Mola wa ‘Arshi tukufu.”[1]

Akajitakasa Mwenyewe (Subhaanah) kutokamana na hilo kama alivyojitakasa kutokamana na mshirika, mwana, mke, aibu na mapungufu mengine yote kama mfano wa kusinzia, kulala, kuchoka, kuwa na haja, kutaabika kuilinda mbingu na ardhi zote.

[1] 23:116

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn bin Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Iddat-us-Swaabiriyn, uk. 161
  • Imechapishwa: 02/04/2020