Allaah hasifiwi kuchoka kama wanavosema wakristo na mayahudi

Kuhusu kumzulia kwao uongo Allaah, Mitume Yake, Manabii Yake na kumtuhumu Mola wa walimwengu na Mitume Yake kwa mambo makubwa wamefanya kwa wingi sana. Moja katika mambo hayo ni pale waliposema kuwa Allaah alipumzika ile siku ya saba baada ya kumaliza kuumba mbingu na ardhi. Ndipo Allaah akateremsha maneno Yake (Ta´ala) hali ya kuwa ni mwenye kuwakadhibisha pale aliposema:

وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ

“Hakika Tumeumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yake katika siku sita na wala hatukuguswa na uchovu wowote.” (50:38)

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn bin Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hidaayat-ul-Hayaaraa (02/417-418)
  • Imechapishwa: 01/04/2020