al-Khaliyliy amesema:

“Kuhusu dalili za kinakili – za wanaopinga kuonekana kwa Allaah – baadhi zinapatikana katika Qur-aan na zingine katika Sunnah.”[1]

Kisha akasema:

“Katika Qur-aan ni maneno Yake (Ta´ala):

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki na Yeye ndiye anayazunguka macho yote.”[2]

Halafu akasema:

“Dalili hapa ni kwamba (Ta´ala) amejisifu kuwa macho hayamdiriki. Kudiriki maana yake ni kuona. Ikapata kubainika kuwa kutoonekana kwa macho ni sifa ya kidhati yenye kulazimiana Naye (Ta´ala). Lau kungelikuwa kipindi anaonekana basi kujisifu Kwake kungeondoka na mambo yakishakuwa hivo inageuka kuwa kinyume chake ambacho ni kulaumika – Allaah ametakasika na hilo.”

Akaendelea kusema:

“Kwa upande mwingine ni kwamba [hapa] Allaah anaelezea sifa miongoni mwa sifa Zake na maelezo ya Allaah hayabadiliki. Lau ingelibadilika basi kubadilika kwake ingelikuwa ni kumkadhibisha:

وَمَنْ أَصْدَقُ مِنَ اللَّـهِ قِيلًا

“Na nani aliye mkweli zaidi kwa kauli kuliko Allaah?”[3]

Tunasema ni kweli kwamba ni maelezo ambayo hayakubadilika. Allaah amesema kuwa anaonekana lakini hata hivyo katika kuonekana huko hazungukwi (Subhaanahu wa Ta´ala) kutokana na ukubwa Wake. Hivyo ndivyo alivyosema Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Sivyo kama anavyoonelea al-Khaliyliy.

[1] Uk. 68

[2] 06:103

[3] 04:122

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 102
  • Imechapishwa: 14/01/2017