Allaah anasifiwa kuwa katika upande upi?


Swali: Je, ni sahihi kumsifia Allaah ya kwamba Yuko katika upande wa juu?

Jibu: Ndio. Tunatakiwa kuamini hivi na sio kumsifia tu. Tuamini hili ya kwamba Allaah Yuko katika upande wa juu. Lakini hata hivyo sio katika upande ulioumbwa. Kusema “Yuko mbinguni” haina maana Yuko ndani ya mbingu (saba) au mbingu zinambeba na kumzuia. Kusema “Yuko mbinguni” maana yake juu, kwa kuwa neno “mbingu” husemwa kwa kukusudia juu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (63) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13810
  • Imechapishwa: 16/11/2014