Allaah anasifika na sifa ya kunyamaza?

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

30- Abu Tha’labah al-Khushaniy Jurthuum bin Naashir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) amefaridhisha faradhi basi msiyapuuze. Vilevile akaweka mipaka msiivuke. Ameharamisha baadhi ya mambo kwa hivyo usifanye. Kuhusu yale aliyoyanyamazia ni kwa ajili ya huruma Yake kwenu – na si kwamba ameyasahau – kwa hivyo usiyadadisi.”

Wamekosea katika hili wale waliosema kuwa neno hili linatolea dalili ya kuthibitisha sifa ya kunyamaza kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Ni miongoni mwa mambo ambayo hayakuthibiti katika maandiko ya Salaf. Hadiyth hii na mfano wake zinazofahamisha kwamba kunyamaza ni sifa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 424
  • Imechapishwa: 13/05/2020