Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ

“Siku utakapofunuliwa muundi na wataitwa kusujudu lakini hawatoweza.” (68:42)

Je, Aayah hii ni miongoni mwa Aayah za sifa za Allaah?

Jibu: Mguu umethibiti kwa Allaah (´Azza wa Jall) katika Hadiyth Swahiyh. Ni mionogni mwa sifa za dhati kutokana na Hadiyth Swahiyh.

Ama kuhusu Aayah hii kuna uwezekano ikawa ndio au hapana. Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) anasema kuwa Aayah hii sio katika Aayah za sifa.

يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ

“Siku utakapofunuliwa muundi…” (68:42)

bi maana ugumu wa hali itavokuwa na sio miongoni mwa Aayah za sifa. Wengine wanasema kuwa ni miongoni mwa Aayah za sifa na ndani yake kuna uthibitisho wa Allaah kuwa na mguu. Allaah ndiye Anajua zaidi. Kwa hali yoyote kuna Hadiyth imekuja Swahiyh inayothibitisha Allaah kuwa na mguu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-1-30.mp3
  • Imechapishwa: 09/08/2020