Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema kwa vile Allaah Ana Sifa ya kucheka basi ni lazima kumthibitishia mdomo? Je, maneno yake ni sahihi?

Jibu: Haya ni maneno batili na ya kipumbavu kwa haki ya Allaah. Sisi tunasema kuwa Allaah Anacheka pasina kujua namna ya kucheka Kwake. Vilevile Anazungumza pasina kusema Anazungumza namna gani kama ni kwa ulimi, mdomo na mengine. Huku ni kuingia kwenye namna. Kunamthibitishia Allaah maneno kulingana na Yeye. Hatuvuki hili.

Mimi ninakutahadharisheni na upetukaji kama huu! Msivuki ibara za Salaf na ibara za Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_05.mp3
  • Imechapishwa: 30/06/2018