Allaah anakubali kilicho chema tu

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

10- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swallla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) ni Mwema na anakubali kilicho chema tu.”

Katika Hadiyth hii kuna matahadharisho makubwa, matishio na woga kwa kila neno au tendo au I´tiqaad chafu yasiyowafikiana na Shari´ah. Chema ni kile kilichotakasika na kasoro. Kitu kikubwa kinachotia kasoro matendo, ni mtu kumshirikisha Allaah (Jalla wa ´Alaa) na badala yake mu akakusudia [katika matendo yake] dunia.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 193
  • Imechapishwa: 17/05/2020