Allaah Ana Sifa Ya Kuwa Na Sura


Swali: Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah Amemuumba Aadam kwa Sura Yake.”

Je, makusudio ni Sura ya Allaah?

Jibu: Bila ya shaka. Kuna Riwaayah nyingine:

“Allaah Amemuumba Aadam kwa Sura ya Ar-Rahmaan.”

Imekuja namna hii katika Riwaayah sahihi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ana Sura, kama ilivyokuja katika Hadiyth:

“Nimemuona Mola Wangu katika Sura nzuri.”

Allaah Ana Sura.

Swali: Je, inajuzu kuiwekea taawili Sura sehemu hii?

Jibu: Hapana. Hadiyth inabaki katika maana yake na matamshi yake. Haibadilishwi.

Shaykh Hamuud at-Tuwayjiriy (Rahimahu Allaah) ameandika kijitabu kizuri kuhusu mada hii. Humo amewaraddi wale wanaitilia taawili Hadiyth hii. Kadhalika kuna maneno ya Shaykh-ul-Islaam kuhusiana na hili.

Swali: Je, imesihi kutoka kwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ya kwamba amesema “Kila mwenye kuwekea taawili Hadiyth hii ya Sura, basi huyo ni Jahmiy”?

Jibu: Kwa kweli mimi sijaona maneno ya Imaam Ahmad. Lakini maana yake ni sahihi. Ni kweli kwamba ni Jahmiyah. Hakuna anayepinga Sifa za Allaah (´Azza wa Jalla) isipokuwa Jahmiyyah. Miongoni mwa Sifa Zake ni Sura.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-03-10.MP3
  • Imechapishwa: 16/11/2014