Swali: Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah Amemuumba Aadam kwa sura Yake.”

Je, makusudio ni sura ya Allaah?

Jibu: Bila ya shaka. Kuna Riwaayah nyingine:

“Allaah amemuumba Aadam kwa sura ya ar-Rahmaan.”

Imekuja namna hii katika Riwaayah sahihi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Ana Sura, kama ilivyokuja katika Hadiyth:

“Nimemuona Mola Wangu katika sura nzuri.”

Allaah ana sura.

Swali: Je, inajuzu kuiwekea taawili sura sehemu hii?

Jibu: Hapana. Hadiyth inabaki katika maana yake na matamshi yake. Haibadilishwi.

Shaykh Hamuud at-Tuwayjiriy (Rahimahu Allaah) ameandika kijitabu kizuri kuhusu mada hii. Humo amewaraddi wale wanaitilia taawili Hadiyth hii. Kadhalika kuna maneno ya Shaykh-ul-Islaam kuhusiana na hili.

Swali: Je, imesihi kutoka kwa Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ya kwamba amesema “Kila mwenye kuwekea taawili Hadiyth hii ya sura, basi huyo ni Jahmiy”?

Jibu: Kwa kweli mimi sijaona maneno ya Imaam Ahmad. Lakini maana yake ni sahihi. Ni kweli kwamba ni Jahmiyah. Hakuna anayepinga sifa za Allaah (´Azza wa Jalla) isipokuwa Jahmiyyah. Miongoni mwa sifa Zake ni Sura.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-03-10.MP3
  • Imechapishwa: 16/11/2014