Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah):

“Ameumba viumbe kwa elimu Yake.”

Hakika Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ameumba viumbe kwa elimu Yake. Hafichikani na kitu sawa ardhini na mbinguni. Yeye juu ya kila kitu ni Mjuzi. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ

“Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.” (08:75)

أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ

“Kwani hajui Yule Aliyeumba na hali Yeye ni Mwenye kuendesha mambo kwa utulivu, Mjuzi.” (67:14)

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚوَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُون

“Na Kwake Pekee zipo funguo za ghayb, hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini; na halianguki jani lolote ila Hulijua, na wala [haianguki] punje katika viza vya ardhi, na wala kilichorutubika na wala kikavu isipokuwa [kimeandikwa] katika Kitabu kinachobainisha. Naye Ndiye Anayekufisheni usiku [mnapolala] na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliopangwa. Kisha Kwake Pekee ni marejeo yenu, kisha Atakujulisheni kuhusu yale yote mliyokuwa mkiyatenda.” (06:59-60)

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/96)
  • Imechapishwa: 31/05/2020