Swali: Umesema kuwa Allaah Anafanya shari lakini sio kwa ajili ya kutaka hiyo shari, bali Anafanya hivo kwa hekima. Kutokana na maneno ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah najua kuwa Allaah Hafanyi shari lakini anaikadiria na kuipanga…

Jibu: Ndugu! Anaumba shari. Allaah ndiye Muumbaji wa kila kitu; kheri na shari. Viumbe vyote ni vya Allaah. Lakini Anaumba shari kutokana na hekima. Kwa nisba Yake sio shari isipokuwa kwa nisba ya watu ndio anaona na inakuwa ni shari. Ama kwa nisba ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) sio shari, bali Anafanya hivo kutokana na hekima. Anaumba kufuru na imani, maasi na utiifu. Hakuna kitu isipokuwa ni kiumbe cha Allaah. Lakini Anafanya hivo kutokana na hekima.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-6-2.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014