Allaah ametuumba kwa ajili ya majaribio

Swali: Ni ipi hukumu ya kusema kwamba Allaah hakutuumba isipokuwa kwa ajili ya mitihani na majaribio?

Jibu: Allaah (Ta´ala) amesema:

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا

“Ambaye ameumba kifo na uhai ili akujaribuni ni nani kati yenu mwenye matendo mema zaidi.”[1]

Kuna majaribio katika ´ibaadah na utiifu. Mwenye kutii basi ana Pepo na mwenye kuasi ana Moto.

[1] 67:02

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191047#191047
  • Imechapishwa: 08/09/2019