Allaah amesalimika na mapungufu na kasoro zote

Allaah amesalimika kutokamana na kila kasoro, upungufu na jambo lenye kusemwa vibaya. Kwani hakika Yeye anao ukamilifu wa moja kwa moja kwa njia zote. Ukamilifu Wake umelazimiana na dhati Yake. Hauwi isipokuwa hivo.

as-Salaam limebeba kusalimika kwa matendo Yake kutokamana na mchezo, dhuluma na kukhalifu hekima, kusalimika kwa sifa Zake kutokamana na kufanana na sifa za viumbe, kusalimika kwa dhati Yake kutokamana na kila upungufu na kasoro na kusalimika kwa majina Yake kutokamana na kila chenye kusemwa vibaya. Kwa hiyo jina as-Salaam ndani yake kuna kumthibitishia ukamilifu wote na kumtakasia mapungufu yote.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Ahl-idh-Dhimmah (01/414)
  • Imechapishwa: 31/03/2020