“Allaah amekuongoza wewe na hakuniongoza mimi”

Swali: Baadhi ya watu wanasema kwamba hawakuwa wakweli kwa Allaah na pindi baadhi watu wanapowalingania kufanya matendo mema wanasema kuwa Allaah amewaongoza wao na hakumwongoza yeye.

Jibu: Hili ni batili. Ni kujengea hoja kwa Qadar. Mtu anatakiwa kumwambia yule anayemlingania katika uongofu:

جزاك الله خيراً

“Allaah akujaze kheri.”

Amwahidi kheri na kwamba Allah akimjaalia atafanya na atapambana na nafsi yake. Ama kutumia hoja kwa Qadar haifai kwake kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 26/06/2021