Allaah ameamrisha aabudiwe Yeye pekee

Swali: Baadhi ya waabudu makaburi au washirikina wa leo wanafupiza ´ibaadah katika swalah pekee na kwa ajili hiyo hawaswali kwa ajili ya mwengine asiyekuwa Allaah ingawa watawafanyia mengine kama vile kuchinja, kuomba du´aa na kutaka uokozi.

Jibu: Haya ni kutokana na ujinga wao. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ

“Mola wako ameamuru kwamba: “Msiabudu isipokuwa Yeye pekee.”[1]

فَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ

“Basi Mimi tu pekee niogopeni.”[2]

فَإِيَّايَ فَاعْبُدُونِ

”Basi Mimi tu pekee niabuduni.”[3]

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ

”Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu”[4]

Hakufanya ´ibaadah ikawa maalum katika swalah pekee. Amesema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Sikuumba majini na watu isipokuwa waniabudu.”[5]

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ

“Muombeni Mola wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye hawapendi wenye kuvuka mipaka.”[6]

[1] 17:23

[2] 16:51

[3] 29:56

[4] 02:21

[5] 51:56

[6] 07:55

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 56
  • Imechapishwa: 23/06/2019