Allaah alikuwa juu ya ´Arshi kabla ya kulingana juu Yake

Huenda mtu akasema hali ya kuuliza ni vipi mtu atasema kuwa Allaah yuko juu ya mbingu ambazo zilikuwa moshi na kwamba yuko juu ya ´Arshi na kwamba hakuacha hata siku moja kuwa juu ya viumbe Wake, kama alivyoeleza Mwenyewe, kutasemwa kuwa anashuka katika mbingu ya chini ya duniani kisha akapanda na wakati huohuo Yeye (Subhaanah) hakuacha kuendelea kuwa juu ya ´Arshi. Kupanda Kwake juu ni katika aina ya kushuka Kwake. Ikiwa katika kushuka Kwake (Subhanaah) hakuna chochote katika viumbe Vyake kinachokuwa juu yake, anapanda pasi na chochote kutangulia kuwa juu Yake.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Hadiyth-in-Nuzuul, uk. 147
  • Imechapishwa: 04/03/2019