Mtu anapomuombea mwenzake du´aa ya kuwa na umri mrefu afungamanishe hilo na neno “utiifu” kwa kusema “Allaah aurefushe umri wako katika kumtii”. Hili ni bora zaidi. Ama kusema “Allaah aurefushe umri wako” peke yake, hii sio du´aa [nzuri]. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mbora wenu ni yule ambaye umri wake unakuwa mrefu na matendo yake yanakuwa mazuri. Muovu wenu ni yule ambaye umri wake unakuwa mrefu na matendo yake yanakuwa mabaya.”

Umri ukiwa mrefu juu ya shari, hii ni shari na sio kheri. Umri ukiwa mrefu juu ya wema, hili ni kheri. Tumezowea kusema:

“Allaah Akurefushie umri wako.”

Hivyo inatakiwa kusema:

“… katika kumtii”

ili kupatikane faida na du´aa iwe na kheri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/101)
  • Imechapishwa: 31/05/2020