Aliyosema al-Khaliyliy juu ya udhahiri wa maneno ya Mtume

Tunamwambia mwandishi, al-Khaliyliy, yafuatayo:

Hivi kweli humchi Allaah kwa maneno yako uliyosema ambayo kwayo unayapinga maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale uliposema:

“Kuchukua udhahiri wa Hadiyth ya Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy zilizoko katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na Muslim yanarudishwa na akili na yanakadhibishwa na dalili.”[1]

Huku ni kuwa na ujasiri kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ni matamshi ya aibu kabisa yanayorudisha maneno ya mkweli mwenye kusadikishwa ambaye hatamki kwa matamanio yake na hayakuwa ayasemayo isipokuwa ni Wahy anaoteremshiwa.

Hakika jambo hili, wewe mwanamume, ni la khatari! Unahitaji kufanya tawbah ya kweli itayokutoa katika ´Aqiydah mbovu na fitina ya upindaji. Allaah amesema:

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije ikawapata fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo.”[2]

Atambue yule mwenye kununua upotevu kwa uongofu ya kwamba kupingana na Allaah kwa kurudisha dalili za Kitabu Chake na kutangulia mbele ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kupingana na Sunnah zake kwa maoni yenye kuoza na mienendo mibaya ni kwenda kinyume kuliko wazi kabisa.

[1] Uk. 56

[2] 24:63

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 95
  • Imechapishwa: 14/01/2017