Aliyekuja amechelewa asimfuate imamu katika Rak´ah aliyozidisha

Swali: Imamu akizidisha Rak´ah moja na mimi nikapitwa na Rak´ah moja niilipe pamoja naye au nitoe salamu?

Jibu: Imamu akizidisha Rak´ah basi haijuzu kumfuata. Ni lazima kwa maalum kumzindua na yule mwenye kujua hilo aseme “Subhaan Allaah.” Akirudi ni sawa. Vinginevyo mswaliji akae chini mpaka pale atapotoa salamu pamoja naye. Aliyekuja amechelewa akijua kuwa ni Rak´ah yenye kuzidi basi asimfuate. Baada ya hapo ndio aswali Rak´ah nyingine moja.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 16/08/2019