Aliyefanyiwa uchawi haandikiwi dhambi?


Swali: Je, mtu ambaye amefanyiwa uchawi anapewa udhuru katika matendo yake yote kama kufanya machafu na kuacha swalah ya mkusanyiko na Fajr?

Jibu: Maadamu yuko na akili zake timamu anahesabiwa kwa matendo yake yote. Ama akili zake zikimtoka na akawa kama mwendawazimu asiyekuwa na akili huyu hahesabiwi. Isipokuwa katika mambo anayoharibu; akiua mtu na akiharibu mali za watu anatakiwa kulipa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13965
  • Imechapishwa: 13/04/2018