´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) aliwapiga vita majini?


Swali: Je, ni sahihi kwamba imaam ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) aliwapiga vita majini? Hayo yametajwa katika kitabu “Ghazawaat-ul-Imaam ´Aliy” na kwamba aliwapiga vita mpaka akawafikisha katika ardhi ya saba. Unasemaje juu ya kitabu hicho?

Jibu: Yote haya hayana msingi. Hakuwapiga vita majini na wala hakukutokea kitu katika mambo hayo. Haya ni batili, uongo na mambo yaliyozuliwa na watu. Abul-´Abbaas Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ametaja jambo hilo na akasema kwamba ni uongo usiokuwa na msingi wowote na kwamba ni katika uongo uliozuliwa na waongo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/277)
  • Imechapishwa: 16/07/2021