Alipe yule ambaye Ramadhaan imempita kwa miaka mingi?

Swali: Ni ipi hukumu ya muislamu ambaye Ramadhaan imempita kwa miaka mingi pasi na kufunga na bila ya kikwazo lakini hata hivyo ni mwenye kutekeleza faradhi nyenginezo? Je, ni lazima kuzilipa pale atapotubia?

Jibu: Sahihi ni kwamba hatozilipa pale atapotubia. Kwa kuwa kila ´ibaadah imetengewa muda maalum mtu atapokusudia kuzichelewesha mpaka nje ya wakati wake pasi na udhuru, basi Allaah hazikubali kutoka kwake. Kujengea juu ya hili hakuna faida yoyote ya kuzilipa. Lakini hata hivyo anatakiwa kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na akithirishe kutenda matendo mema. Allaah anamsamehe yule mwenye kutubia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/87)
  • Imechapishwa: 07/06/2017