Swali: Mtu akiacha baadhi ya swalah za faradhi kisha baadaye akatubia. Je, ni lazima kwake kuzilipa?

Jibu: Akiziacha kwa kukusudia hatakiwi kuzilipa. Hakuna dalili ya kwamba anatakiwa kuzilipa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atayepitikiwa na usingizi kwa swalah au akasahau basi aiswali pale atapokumbuka.”

Ni dalili inayothibitisha kuwa yule mwenye kuiacha kwa kukusudia hatakiwi kuilipa. Lakini anatakiwa kutubia kwa Allaah na ahifadhi swalah. Kwa sababu kule kuacha kwake kwa kukusudia amekufuru. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ahadi iliyopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi yule mwenye kuiacha amekufuru.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (2621), an-Nasaa’iy (463) na Ibn Maajah (1079). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (71) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah26-07-1438h%20-%20Copy.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2017