Alikuwa hatoi zakaah ya dhahabu kwa ujinga na sasa dhadhabu yote imekwisha


Swali: Kuna mwanamke alikuwa na dhahabu na wala hatoi Zakaah kwa kutokujua. Na kwa sasa hakubaki na kitu. Je, ni juu yake kutoa Zakaah sasa au afanye nini?

Jibu: Ndio. Ni wajibu kwake kutoa Zakaah ikiwa yuko na uwezo wa kufanya hivyo, la sivyo itabaki juu ya dhimmah yake. Kwa kuwa hii ni haki ya mafukara. Huu ndio wajibu wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://olamayemen.net/default_ar.aspx?id=662
  • Imechapishwa: 08/03/2018