Swali: Kuna kijana mmoja ambaye bado hajabaleghe alifikiwa na Ramadhaan ambapo akafunga. Mwaka wa kufuata akabaleghe pamoja na hivyo akaendelea kuwa anafanya punyeto mchana wa Ramadhaan. Hata hivyo alikuwa hajui hukumu. Hajui ni siku ngapi alifanya punyeto. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Kusema kwamba alikuwa anafanya punyeto bado hajabaleghe ina maana kwamba alikuwa hatokwi na manii. Kikawaida punyeto inampelekea mtu kutokwa na manii hata kama ana miaka kumi peke yake. Alikuwa hajui hukumu na anadhani kuwa puneyo haifunguzi. Kwa ajili hiyo si lazima kwake kulipa siku zake. Allaah (Ta´ala) amesema:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

Allaah akasema:

“Nimefanya hivo.”

[1] 02:286

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/234-235)
  • Imechapishwa: 27/05/2019