Swali: Wakati nilipokuwa na miaka ishirini na tano katika Ramadhaan nilikuwa nikifanya nikijichua sehemu ya siri na sikuwa najua kama ni haramu na kwamba kitendo hicho kinaharibu swawm. Hivi sasa sijui ni siku ngapi niliharibu swawm yangu. Nifanye nini?

Jibu: Ni lazima kwako kutubu na kuomba msamaha. Ni wajibu vilevile kukadiria zile siku unazodaiwa mpaka pale utapokuwa na dhana yenye nguvu kwamba umetekekeza yale unayodaiwa. Kwa mfano ukiwa ni mwenye shaka kama ni siku tano, sita, saba, nane, tisa au kumi basi fanya kuwa ni siku kumi mpaka uwe na dhana yenye nguvu kuwa umetekeleza wajibu wako.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 21/11/2018