Alikusanya swalah ya ijumaa pamoja na ´Aswr mwaka mmoja ulopita

Swali: Nilikusanya swalah ya ´Aswr pamoja na swalah ya ijumaa nilipokuwa safarini mwaka mmoja ulipita. Kisha baadaye nikaja kujua kuwa kitendo hichi hakijuzu. Je, ni lazima kwangu kuirudi swalah ya ´Aswr?

Jibu: Ndio, irudi swalah ya ´Aswr.

Swali: Nikiirudi niiswali hali ya kuifupisha au hali ya kuikamilisha?

Jibu: Rudi kuilipa hali ya kuikamilisha. Kinachozingatiwa ni pale wakati utakapoirudi. Ikiwa wakati wa kuirudi si msafiri, basi utatakiwa kuirudi kikamilifu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (97) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igatha26-02-1440-h.mp3
  • Imechapishwa: 11/05/2019