Alifunga wakati wa hedhi pasina kujua kuwa haifai


Swali: Msichana huyu alipojiwa na hedhi kwa mara ya kwanza katika Ramadhaan ambapo alikuwa na miaka kumi na tatu alikuwa akifunga na kuswali na hakulipa yale masiku ambayo alipata hedhi ndani yake pamoja na kuzingatia ya kwamba hakuwa anajua kuwa ni haramu kufunga kipindi cha hedhi na kwamba anatakiwa kulipa baada ya Ramadhaan. Katika kipindi cha miaka hii kuna masiku mengi yaliyompita. Je, ayalipe?

Jibu: Pili: Haijuzu kwa mwenye hedhi kufunga wala kuswali wakati wa hedhi yake. Yale yaliyofanywa na mwanamke huyu aliyetajwa kufunga na kuswali wakati wa hedhi ni kosa. Ni wajibu kwake kutubu kwa Allaah na kumuomba msamaha. Si mwenye kupewa udhuru kwa ujinga juu ya hukumu ya mambo kama haya. Kwa sababu lililo la wajibu kwake ni yeye kuuliza.

Pili: Ni wajibu kwake kulipa masiku yote ambayo hedhi ilimjia katika Ramadhaan. Ni mamoja hayo yalikuwa katika Ramadhaan moja au Ramadhaan nyingi. Kufunga kwake wakati wa hedhi si sahihi. Pamoja na kufunga ni wajibu kwake vilevile kulisha masikini kwa kila siku moja takriban 1,5 kg katika chakula kilichozoeleka katika mji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/189-190)
  • Imechapishwa: 18/05/2018