Aliacha kufunga Ramadhaan kwa sababu ya maradhi kisha akafa


Swali: Kuna mtu alikuwa mgonjwa katika mwezi wote wa Ramadhaan na akafa hospitalini na hakulipa kitu na wala hakutolewa kafara. Ni kipi kinachomlazimu hivi sasa? Je, afungiwe au atolewe kafara? Tunaomba faida.

Jibu: Ikiwa maradhi haya yaliyomshika katika Ramadhaan ni maradhi ambayo watu hukata tamaa juu ya kupona kwake, basi lililo la wajibu ni yeye kutolewa chakula na hatofungiwa. Ama ikiwa ni maradhi ambayo yanatarajiwa kupona lakini hata hivyo yakawa mazito kwake mpaka alipofariki, basi haimlazimu kulipa wala kulisha. Kwa sababu mtu ambaye kaacha kufunga kwa maradhi ambayo yanatarajiwa kupona, anakadiriwa kuwa atafunga. Iwapo maradhi hayo yataendelea, basi hatotakiwa kulipiwa. Kwa sababu imekadiriwa kuwa atafunga pale atapoweza.

Lakini katika hali kama hii, ikiwa mwanzoni mwa Ramadhaan yalikuwa ni maradhi yanayotarajiwa kupona na baada ya nusu yake yakageuka kuwa maradhi yasiyotarajiwa kupona na mwishowe akafa, katika hali hii tunasema kuwa wamtolee chakula katika yale masiku ya mwisho ambapo maradhi yaligeuka kutotarajiwa kupona. Ama yale masiku ya mwanzo ndio yanayotakiwa kulipwa. Kuhusu yale ambayo hakuweza yanaanguka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/943
  • Imechapishwa: 10/05/2018