Alama ya kwanza ya Ahl-ul-Ahwaa´ ni mfarakano. Ni wenye kufarikiana kwa sababu wanafuata matamanio yao. Baadhi ya wanachuoni wanasema:

“Kila suala lililozuka katika Uislamu na likasababisha watu kufarikiana pasi na tofauti hiyo kusababisha wakaanza uadui na kuchukiana ni katika Uislamu. Na kila suala lililozuka na likasababisha uadui, kuchukiana, kususana na kukatana basi halina chochote kuhusiana na dini.”[1]

Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ ni watu wa mfarakano ambao wanakuja katika jamii ya Ahl-us-Sunnah ambao raia wamefungamana na watawala wao na asiyekuwa msomi amefungamana na wanachuoni wao. Wanakuja katika jamii kama hii iliyofungamana na kuwa na umoja na kuifarikisha na kuitenganisha. Wanawafanya viongozi kuwachukia wananchi na wananchi kuwachukia viongozi. Wanawafanya wanachuoni kuwachukia wasiokuwa wasomi na wasiokuwa wasomi kuwachukia wanachuoni na kadhalika. Ndivyo walivyo Ahl-ul-Bid´ah.

Ukipeleleza mfarakano na tofauti basi utaona chanzo chake inatokamana na Ahl-ul-Bid´ah. Khawaarij walijitokeza mwanzoni mwa Uislamu na wakaupasua Uislamu. Mpaka hii leo donda hilo halijapona.

Kadhalika al-Ikhwaan al-Muslimuun wametuzukia miaka miwili au mitatu ya nyuma; wametufarikisha na kutugawa, jambo ambalo tunaona athari yake mpaka hii leo.

Hii ni alama ya kwanza ya Ahl-ul-Bid´ah; wanafarikisha.

[1] al-I´tiswaam (3/169) ya ash-Shaatwibiy.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Jarh wat-Ta´diyl ´indas-Salaf, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 09/08/2020