al-Waadi´y kuhusu ugoro


Swali: Ni ipi hukumu ya ugoro na sigara?

Jibu: Ugoro na sigara ni miongoni mwa majanga ambayo waislamu wamepewa mtihani kwayo. Ugoro ni uchafu. Wenye kuutumia wanashuhudia juu ya nafsi zao jambo hili; ya kwamba ni uchafu na hauna faida yoyote ndani yake.

Sigara pia ni yenye madhara zaidi. Huenda hata ukamfanya mtu kupatwa na kansa. Jamaal-ud-Diyn al-Afghaaniy amepatwa na kansa mdomoni mwake kwa sababu ya sigara. Huenda mtu ukamletea kifua kikuu. Kuhusu kifua kikuu ni kitu ambacho hutakiwi kuuliza juu ya ukhatari wake. Kwa hali yoyote ni yenye kudhuru na haina kheri yoyote ndani yake. Nawaomba ndugu wote kujiepusha nayo. Jengine isitoshe sigara inafanya meno kuwa meusi na inaleta harufu mbaya mdomoni. Tunamshukuru Allaah kuona Allaah amewalinda na mambo ya sigara wale wenye kufuata Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Iko karibu zaidi na uharamu. Kuhusu kutumia dalili ya maneno Yake (Ta´ala):

وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ

“Anawahalalishia vizuri na anawaharamishia maovu.”[1]

Aayah haifahamishi jambo hilo. Ni dalili inayoonyesha kuwa ni machafu yale aliyoharamisha Allaah. Lakini sigara haina kheri yoyote ndani yake. Iko karibu zaidi na uharamu. Muislamu anatakiwa kujiepusha nayo.

[1] 07:157

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3114
  • Imechapishwa: 08/11/2019