Swali 207: Ni lazima kwa yule mwanamke anayeendesha gari afunue uso wake ili aweze kuendesha.

Jibu: Akiwa ni mfanyakazi na anaona kufaa kuonyesha uso basi hakuna neno akafanya hivo. Ingawa mimi sionelei kufaa. Lakini maneno yako kusema kwamba ni lazima afunue uso wake si kweli. Anaweza kuacha wazi sehemu ndogo ya macho yake na akaendesha. Kwa hivo ulivosema si kweli. Kuhusu masuala ya uso na vitanga vya mikono tumekwishayaongelea hapo jana. Lakini nayarudia kwa sababu ni mwenye ujasiri wa kuyataja. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako – na wanawake [wote] wa Waumini – ya kwamba [nje ya nyumbani] wajiteremshie mavazi yao ya juu; hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane [kuwa ni wanawake wa heshima] na wasiudhiwe.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke ni ´Awrah. Pindi anapotoka nje basi shaytwaan humpamba.”

Lakini endapo atakuwa amejitahidi na akawa ni Mujtahidah na mwanachuoni ambapo akaona kwamba uso na vitanga vya mikono si lazima kuvifunika natarajia kuwa hakuna neno. Ana haki ya kufanya Ijtihaad. Hata hivyo anazingatiwa ni mwenye kukosea katika Ijtihaad yake licha ya kwamba wanachuoni wengi wanaona hivo [kujuzu kuonyesha uso].

[1] 33:59

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 409-410
  • Imechapishwa: 25/11/2019