Swali 286: Inafaa kwa muislamu kumuoa mwanamke wa kiyahudi au wa kinaswara?

Jibu: Akiwa ni wa kiyahudi au wa kinaswara basi ni halali kwa andiko la wazi la Aayah ya Qur-aan:

الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ

“Leo mmehalalishiwa vizuri na chakula cha Ahl-ul-Kitaab ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao na wanawake wenye kujiheshimu kwa machafu [wasiozini] miongoni mwa waumini wanawake na wanawake wenye kujiheshimu kwa machafu [wasiozini] miongoni mwa Ahl-ul-Kitaab kabla yenu.” (05:03)

Lakini muislamu anatakiwa kuchukulia lililo salama zaidi. Pale anapotaka kumuoa mwanamke wa kikristo na katika nchi hiyo unaswara ndio wenye nguvu zaidi basi kunakhofu watoto wakageuka  wakristo. Kadhalika akumuoa mwanamke wa kiyahudi basi kunachelewa akawalingania watoto wakawa mayahudi. Mtoto huzaliwa juu ya maumbile salama na baadaye wazazi ndio huwafanya wakawa mayahudi, wakristo au waabudu moto. Kama mwanamke huyo ni mshirikina basi itambulike kuwa kumuoa mshirikina haijuzu na kufunga ndoa na mwanamke wa kushirikina haijuzu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 531
  • Imechapishwa: 30/11/2019