al-Waadi´iy kuhusu ulazima wa kuweka nia katika funga zilizopendekezwa

Swali: Je, imeshurutishwa kuweka nia katika Swawm ya Naafilah?

Jibu: Imeshurutishwa, kwa dalili ya Hadiyth:’

“Hakika ya kila kitendo kinategemea nia.”

Ama Hadiyth:

“Yule asiyenuia swawm (katika Uislamu), hana swawm.”

Ni Hadiyth dhaifu haikuthibiti kwa Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hata kama imesahihishwa na baadhi ya wanachuoni wetu.

Pia isitumiwe kama dalili Hadiyth ya Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwa baadhi ya wake zake akasema: “Je mna chakula”? Akaambiwa “Hapana”. Akasema “Basi nimefunga”.

Kwa kuwa alikuwa amenuia kufunga. Vilevile inajuzu kwa aliyefunga funga iliyopendekezwa kula. Kwa hiyo isitumiwe kama dalili kuwa Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliweka nia wakati ule. Hadiyth:

“Hakika ya kila kitendo kinategemea nia.”

Ni dalili ya kuwa swawm haisihi kukishapita sehemu ya mchana.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbil.net/fatwa.php?fatwa_id=1612
  • Imechapishwa: 26/08/2020