Swali: Tunaoma kalima kwa wanaume na wanawake kuhusu ukewenza?

Jibu: Hili ni jambo muhimu enyi ndugu zetu:

فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً

“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake; wawili au watatu au wanne. Mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi [oeni] mmoja.” (04:03)

Hapa ni pale ambapo mwanaume anaimania nafsi yake ya kuwa atafanya uadilifu. Hili ni jambo la kwanza. Jambo lingine awe yuko na uwezo. Ama hali yake ikiwa ni ile ya watoto wako ni wagonjwa na amekosa hata pesa za matibabu, kisha baada ya hapo anataka kuoa mke wapili, watatu au wanne naye isitoshe ni mwanafunzi, hili litamshughulisha enyi ndugu. Allaah Akimfungulia milango ya riziki na akamrahisishia njia ya mali, hakuna ubaya akafanya hivyo bali tunamnasihi kufanya hivyo. Hali kadhalika, awe ni mwenye kujiaminia nafsi yake ya kutomili kwa mwanamke mmoja. Na wala haijuzu kwa mwanaume wala mwanaume kuharamisha Aliyohalalisha Allaah (Ta´ala). Lakini inatakikana kama tulivyotangulia kusema, ajilazimishe kufanya uadilifu na awe na uwezo wa kuongeza mke wapili, watatu au wanne. Na tunamuomba Allaah (Ta´ala) Awawekee wepesi ndugu zetu ambao hawajaoa. Tunamuomba Allaah Awawekee wepesi. Na ni kweli ya kuwa, kuna wanawake Sunniy Dammaaj na nje ya Dammaaj na wanatamani kuolewa na watafutaji elimu katika Ahl-us-Sunnah. Lakini pengine mama yake akawa amtenza ndugu na kumwambia: “Mume wa msichana wangu hatokuwa na mke isipokuwa mmoja tu. Atakuwa na gari, makumbusho (museum) n.k.”

Pengine wazazi wa msichana huyu wakawa wanamshaji´isha katika hili na wakamwambia mwanafunzi aliyekuja kuchumbia: “Tunasikitika! Tumempa fulani kwa utajiri wake na wewe umekosa kwa ajili wewe ni mwanafunzi.” Masikini, huenda mwanafunzi huyu hana lolote zaidi ya kilemba chake, kanzu yake na suruwali yake. Wapi atatoa pesa zote hizi? Tunachowanasihi ndugu zetu wasaidizane na ndugu zao ili kutengeneza familia njema na yenye Imani. Na ni juu yako mzazi kumchagulia msichana wako mwanaume mwema, akimpenda atamkirimu na akifikia kumchukia hatomdhulumu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2632
  • Imechapishwa: 14/02/2018