Swali: Kuchinja katika maulidi, kusherehekea usiku wa ishirini na saba Rajab, sikukuu ya Hijrah, sikukuu ya kuzaliwa kwa mama na sikukuu ya mapinduzi ni katika mambo ya kipindi cha kikafiri?
Jibu: Sikukuu yoyote, mbali na ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adwhaa na ijumaa ambayo ni sikukuu ya wiki, zilizobaki zengine zote ni katika mambo ya kipindi cha kikafiri ambazo hazikuja katika Kitabu na Sunnah.
- Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2992
- Imechapishwa: 05/09/2020