Abu ´Abdir-Rahmaan analingania katika Jamaa´at-ul-Jihaad. Hili ni kosa. Sisi tuko katika nchi ya Kiislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muumini hatoacha kuwa na wasaa katika dini yake muda wa kuwa hajamwaga damu ya haramu.”

Imepokelewa na al-Bukhaariy kutoka katika Hadiyth ya Ibn ´Umar.

Allaah (´Azza wa Jalla) amesema:

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

“Atakayemuua muumini kwa kusudi, basi malipo yake ni [Moto wa] Jahannam, atakaa humo kwa muda mrefu na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamuandalia adhabu kuu.” (04:93)

Ni kama tulivosema nchi ni ya Kiislamu. Serikali, mbali na majanga ilio nayo, ni ya Kiislamu. Sisi hatuko radhi na kitu chochote kinachoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah, hata hivyo hatuwezi kuwakufurisha.

Suruuriyyah ni wajinga. Wanaeneza ufisadi na ni wajinga. Wanakuja na maneno matupu. Jamaa´at-ul-Jihaad ni kundi la magari. Wako nyuma tu ya magari ya Usaamah bin Laadin. Wanapopata gari moja, wanataka gari nyingine. Ni kundi liko nyuma ya dunia. Kwa nini wanasema kwamba wao ni “Jamaa´at-ul-Jihaad”? Ni maneno matupu. Nyinyi ni kundi linaloeneza tu ufisadi na sio kundi linalotoka katika Jihaad. Ni kundi lililo nyuma ya kutaka kupata vyeo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=37 Tarehe: 1420-09-27/2000-01-04
  • Imechapishwa: 28/03/2024