al-Waadi´iy kuhusu Saudi Arabia na Abu Muhammad al-Maqdisiy

Swali: Kuna tetesi kwamba wewe ndiye ambaye umeandika dibaji ya al-Maqdisiy ambapo anaikufurisha nchi. Je, upi ukweli wa hayo?

Jibu: Hayo ni uongo. Mimi hapo kabla nilikuweko al-Madiynah na baada ya kutiwa jela na nilikuweko ar-Riyaadh. Nimetoka hali ya kuwa si mwenye kukufurisha serikali ya kisaudi. Ni vipi nitaikufurushi ilihali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ambaye atamwambia ndugu yake ”ee kafiri!” basi itampata mmoja wao.”

Haijuzu kwetu kuikufurisha serikali hiyo. Ni nchi ya Kiislamu.

Swali: Ee Shaykh! Unasemaje juu ya bwana mmoja anayeitwa Abu Muhammad al-Maqdisiy? Ni yepi maoni yako juu yake? Je, ni katika wanachuoni?

Jibu: Bwana huyu huandika vitabu na ndani yake mna makosa mengi. Wakati mmoja alituagizia kitabu. Kama sikusahau ilikuwa ”I´daad-ul-Fawaaris bi Tark-il-Madaaris” au kingine – Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kwa vovyote haikuwa kitabu ”al-Kawaashif al-Jaliyyah”. Hakukiri kuwa yeye ndiye ambaye alikiandika. Alinipa ili nikisome. Kipindi hicho sikuwa na wakati, nikampa nacho ndugu mwenye umaizi, ambaye ni ´Abdul-´Aziyz al-Bura´iy. Akabainisha makosa yaliyomo ndani yake ikiwa ni kama nasaha kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Baada ya hapo nikamwagizia nacho. Ndipo akataka kumjibu ´Abdul-´Aziyz al-Bura´iy. Nikamwambia:

”Bwana huyu ni mjinga na mwenye jeuri. Achana naye. Haitakikani kwetu kupoteza wakati wetu kwa ajili yake.”

Tatizo ni kwamba watu wakimuona mtu ana hamasa juu ya Uislamu, basi wanafikiri kuwa ni mwanachuoni. Kuna watu wengi wanaofikiri kuwa ni katika wanachuoni ilihali ukweli wa mambo si katika wao. Bwana huyu si katika wanachuoni.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://sahab.net/forums/showthread.php?t=296060 http://www.youtube.com/MuslimerSverige2#p/u/2/0r2Q8z-Gbcw
  • Imechapishwa: 02/12/2020