al-Waadi´iy kuhusu mwanamke kuwa mbele anapowaongoza wenzake katika swalah


Swali: Mwanamke akiwaongoza wanawake katika Swalah, je, asimame mbele ya wanawake au asimame katikati yao kama alivyofanya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha). Aliswalisha watu, akasimama katikati yao. Kasema hili Imaam al-Bayhaqiy? Je, hili limethibiti kwake? Na kama limethibiti, je inafaa kuitumia kama hoja?

Jibu: Ndio limethibiti. Na kuna upokezi mwingine unaofanana na wa ´Aaishah ya kwamba Ummu Salamah alifanya hivyo. Ingawa kitendo cha ´Aaishah na Ummu Salamah vimethibiti, lakini si hoja. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

Na Hadiyth hii inamgusa mwanaume na mwanamke. Kama ilivyo katika Kauli Yake (Ta´ala):

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ

“Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah.” (02:110)

Hii inamgusa mwanaume namwanamke. Lililo la dhahiri ni kuwa, Sunnah ni mwanamke atangulie mbele ya wanawake kama afanyavyo Imamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=778
  • Imechapishwa: 08/03/2018