Swali: Je, mwanamke anaweza kuondosha nywele za usoni mwake na za mwili wake wote isipokuwa tu za kichwani tu?

Jibu: Tunachomnasihi asiziondoshe, isipokuwa tu ikiwa kama yuko na ndevu. Hakuna ubaya akaziondosha. Kwa kuwa akiziondosha kwa mara ya kwanza, zitaongezeka na kuwa nyingi zaidi. Isitoshe zitakuwangumu na mbaya ilihali angeliziacha zingekuwa laini. Tunamnasihi asifanye hivyo, na lau atafanya hivyo hakuna neno. Hakuna dalili inayoharamisha na hili – In Shaa Allaah – haliingii katika kubadilisha maumbile ya Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1556
  • Imechapishwa: 07/03/2018