al-Waadi´iy kuhusu mahali pa mikono baada ya Rukuu´

Swali 265: Ni yepi maoni yenye nguvu kuhusu kuweka mikono miwili baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´?

Jibu: Ni jambo sahali. Hakukuthibiti dalili sahihi na ya wazi kuhusu jambo hili. Kwa hivyo sisemi kuwa ni Bid´ah na wala sisemi pia kuwa ni Sunnah. Lakini hata hivyo ni jambo la ki-Ijtihaad. Mwenye kuweka mkono wake wa kuume juu ya mkono wake wa kushoto juu ya kifua baada ya kuinuka kutoka katika Rukuu´ ametendea kazi yale yaliyoenea. Na vilevile mwenye kuachia mikono ametendea kazi Hadiyth ilioko katika “as-Swahiyh” ya Muslim.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 500
  • Imechapishwa: 29/11/2019